Wajibu kwa Mungu
Kuzingatia kanuni za kiroho, kuwa mwaminifu kwa dini inayozieleza na kukubali wajibu unaotokana nazo.
Dodoma Scouts
Dira yetu ni kuwa harakati ya vijana yenye kuhamasisha zaidi na inayojumuisha wote, ikitoa uzoefu wa kujifunza wenye kuleta mabadiliko kwa kila kijana.
Dhima yetu ni kuchangia elimu ya vijana kupitia mfumo wa maadili unaotokana na Ahadi na Sheria ya Skauti. Kupitia Skauti, tunajenga dunia bora ambamo watu wanajitambua na kujikamilisha kama mtu mmoja mmoja na kutekeleza wajibu wenye manufaa katika jamii.
Harakati yetu imejengwa juu ya kanuni zifuatazo:
Kuzingatia kanuni za kiroho, kuwa mwaminifu kwa dini inayozieleza na kukubali wajibu unaotokana nazo.
Uaminifu kwa nchi yetu sambamba na kukuza amani, uelewano na ushirikiano katika ngazi ya eneo, taifa na kimataifa.
Kuwajibika katika kujiendeleza binafsi.

